Msimamizi wa uchaguzi, jimbo la Hai anawatangazia kuwa kutakua na zoezi la usaili kwa wale wote walioomba nafasi za Msimamizi Mkuu, Msimamizi Msaidizi Na1 na 2 na Karani mwongozaji wa uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 28/10/2020.
Usaili huu utafanyika siku ya Jumapili tarehe 11/10/2020 kuanzia saa (6) sita kamili mchana hadi saa (10) kumi jioni katika shule ya msingi kibaoni iliyoko karibu na stendi kuu ya mabasi Hai Mjini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 27 Hai
Simu: 0272758441
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai