Kampeni ya “Nipe Nafasi Tena” imezinduliwa rasmi katika shule ya sekondari Bomang’ombe wilayani Hai, ikilenga kuwapa wanafunzi nafasi ya pili na kuwapa misaada wanafunzi wanaosoma chini ya mradi wa SEQUIP katika shule ya sekondari bomang’ombe.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Hai, Bi. Hellen Mselem, aliyekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtenadaji Akihutubia wanafunzi na walimu, Bi. Mselem alisema kampeni hiyo ni chachu ya kuwasaidia vijana kuzingatia elimu kama nyenzo ya kufanikisha ndoto zao.
“Nawasihi kila mwanafunzi kutumia nafasi hii kwa bidii na nidhamu. Elimu ndiyo nguzo ya maisha yenu na serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kila mmoja anapata mazingira bora ya kujifunzia,” amesema Bi. Mselem.
Kwa upande wake, Afisa Habari wa Wilaya ya Hai, Bi. Riziki Lesuya, alisema kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuhakikisha vijana wanajitambua na kutumia vizuri nafasi walizonazo.
“Tumefanya haya kwa kushirikiana na wadau mbali mbali nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru wote waliojitoa kwaajili ya hili, radio boma peke yetu hatuwezi ila kwa kushirikiana na wasikilizaji na wadau Mungu katuwezesha. Tunatamani kuona Kampeni hii inaleta mwamko wa kielimu na maadili miongoni mwa wanafunzi,” amesema Bi. Lesuya.
Naye kiongozi wa darasa la SEQUIP, Maico, alitoa shukrani za dhati kwa serikali na wadau waliowezesha kampeni hiyo.
“Kwa niaba ya wenzangu, ninaishukuru boma hai fm kwa kutuletea kampeni hii. Imetupa hamasa kubwa ya kuendelea kusoma kwa bidii na kutokata tamaa licha ya changamoto tunazokabiliana nazo nashukuru sana na Mungu awabariki wote,” amesema Maico.
Kampeni ya “Nipe Nafasi Tena” inatarajiwa kufungwa rasmi mnamo tarehe katika shule ya bomang’ombe sekondari, ikiwa na malengo ya kuongeza mahitaji, kujenga maadili na kuwaandaa vijana kwa maisha bora ya baadaye.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai