Halmashauri ya wilaya ya Hai imeisaini mkata na kampuni ya Nolspan International wenye tahamani ya shilingi bilioni 10.89 kwa ajili ya ujenzi wa soko jipya la Kwasadala mradi unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka 2.
Akizungumza kabla ya kusaini Mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Dionis Myinga amesema serikali imetenga shilingi bilioni 11.6 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo mkandarasi aliyepatikana amekisia kutumia bilioni 10.8 katika ujenzi utakao fanyika kwa miaka miwili na kwamba utekelezaji wake una anza mara baada ya kusaini mkataba.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo Mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko amemwagiza mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anafanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuikamilisha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
“kwetu sisi watu wa Hai hii ni historia hivyo nitasimimia mkataba huu kwa uchu na wivu mkubwa sana, ukakamilike kwa wakati hatutaki kona kona watu wawe sight ,sitocheka na mtu yoyote kwenye huu mradi, kazi ikafanyike amesema Bomboko.
Bomboko pia amemshukuru Mhe.Rais kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi mradi huo utakao badilisha uchumi wa wananchi wa wilaya ya Hai ambao watafanya biashara katika mazingira safi,salama na rafiki kwa kazi zao.
“Kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa soko la Kwasadala ni fedha nyingi sana ambazo kama tungejenga shule ,tungejenga shule 20 kwetu sisi wana Hai kupata fedha nyingi kiasi hiki kwa kutekeleza mradi mmoja ni historia amesisitiza Bomboko.
Akizungumza baada ya Kusaini Mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nolspan International Noel Christopher ameahidi kutekeleza mradi huo kwa ubora na kwa wakati ili kutimiza maono ya serikali kwa wananchi wake.
Tumepata nafasi hii ya kutekeleza ujenzi mkubwa soko hili la kisasa na tutahakikisha kuwa yale maono ambayo serikali ilkuwa nayo yanatimia na kuhakikisha kuwa ile fedha ambayo mhe. Rais ameteoa itaonekana katika soko hiliamesema Christopher.
Soko la Kwasadala kwa sasa linaamika kuhudumia wafanya biashara kutoka mikoa ya Tanga, Arusha, Dar es Salaam,Dodoma na mikoa mingine mingi ya Tanzania ambayo hutegemea mazao ya mboga mboga ,ndizi na matunda kutoka katika soko hilo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai