Wanafunzi waliorejea masomoni baada ya kukatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha wanapaswa kutumia muda wao vizuri na kutambua nafasi waliyopewa ni ya thamani katika kutimiza ndoto walizonazo.
Ameyasema hayo afisa elimu Sekondari wilaya ya Hai wakati wa uzinduzi wa kampeni Maalumu ilitoandaliwa na kituo cha Matangazo cha Radio Boma Hai Fm iiyopewa jina 'Nipe nafasi tena' yenye lengo la kuwaunga mkono wanafunzi wenye changamoto mbalimbali waliorejea masomoni.
Aidha Afisa elimu ambaye ndiye mgeni rasmi kattia uzinduzi huu Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtenadaji Wilaya ya Hai Dionis Myinga, kampeni hiyo ametoa ahadi ya kupatikikana kwa hostel 1 kwa ajili ya wanafunzi wa kike Kwa lengo la kutatua changamoto ya umbali mrefu, utoro na ujauzito wa kujirudia.
Kwa upande wake,Afis Habari wa wilaya ya Hai Riziki Lesuya amewashukuru wadau mbalimbali na wasikilizaji wa Radio Boma waliosaidia kufanikisha uzinduzi wa kampeni hii pia ametoa wito kwa wanaotamani kushiriki katika kampeni hii bado fursa ipo mpaka pale watakapotangaza kufunga rasmi kampeni ya Nipe nafasi tena.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Boma Elisei Msoka ametoa shukrani zake kufuatia uzinduzi wa kampeni hii kwani itawajengea wanafunzi kujiamini vilevile amewataka wanafunzi kutokukata tamaa na kusoma kwa bidii ili wapate matokeo mazuri.
Kampeni ya nipe nafasi tena inalengo la kuunga mkono juhudu za serikali za kuwarejesha shuleni wanafunzi waliocha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni,hali ngumu ya maisha, magonjwa na sababu nyingine mbalimbali, kampeni hiyo imeandaliwa na Radio Boma Fm kwakushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai