Zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Hai limeendelea leo kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jimbo la Hai
Miongoni mwa waliyochukua fomu ni Daniel Mkama Maregesi kupitia chama cha MAKINI, pamoja na Sylvia Dominick Mtenga kutoka chama cha Kijamii. Aidha, wagombea hao wametumia nafasi hiyo kueleza dhamira zao na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake, Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Hai, Aidan Angetile, amethibitisha kuwa kwa siku ya leo fomu za ubunge zimechukuliwa na vyama viwili ambavyo ni chama cha MAKINI na chama cha Kijamii.
Pia ameeleza kuwa vyama vingine ikiwemo NCCR na NRA vimewasilisha majina ya wagombea urais kwa ajili ya uhakiki.
Zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali lilianza tarehe 14 Agosti mwaka huu, na linatarajiwa kukamilika tarehe 27 Agosti 2025. Tume imetoa wito kwa vyama vyote kufika mapema kuchukua na kurejesha fomu ili kuepuka changamoto za muda.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai