Wawekezaji wilaya ya Hai wametakiwa kulinda rasimali zilizopo katika maeneo wanayowekeza pamoja na kutunza mazingira kwa kupanda miti yakutosha ili kuendelea kulinda uoto wa asili.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wilaya ya Hai Ndugu Sospeter Magonera wakati akishuhudia utiaji sain kati ya mwekezaji ambaye ni APKL na chama cha ushirikia cha FONRWA uliofanyika katika shamba hilo lililopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Pia amewataka wawekezaji kuendeleza kuyatunza mashamba hayo ambayo ni zawadi kutoka kwa mungu huku akiwasisitiza kuwa ardhi hiyo iliyotolewa na Mungu isiwagombanishe watu kwa dhuluma na wivu Kwa namna yoyote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya APKL ( African Partnership Kilimanjaro Limited) Ndugu Anold Temba ameishukuru serikali na chama cha ushirika kwa makubaliano ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya mkataba wa shamba hilo lenye Hekari 205 ambazo kati ya hizo 25 zitakuwa ni Shamba Darasa kwaajili ya mafunzo Kwa wanaushirika na Wananchi wengine, na nyingine ni kwaajili ya Kilimo cha Kahawa aina ya Arabica
Amesema kwa kipindi cha miaka kumi wamekuwa wakitoa ajira zaidi ya 940 kila siku na uzalishaji ukiendelea kukua hadi kufikia gunia zaidi ya elfu 3000 kwa mwaka.
Nae Mrajisi wa vyama vya Ushirika Mkoa Bi Jacline Senzigwa ameeleza vipengele mbalimbali kwenye mkataba na kuwaka wanashirika kuchangia pato la taifa na kuwaeleza wawekezaji kuwa wanatakiwa kutenga asilimia 10 kwaajili ya miradi ya jamii jambo ambalo ni takwa na vyama na mkataba kwa lengo la kurudisha kwa jamii na kulinda rasimali.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Eliisi Muro ameiomba Kampuni ya APKL kuzingatia mkataba waliosaini ili kuliendeleza shamba hilo.
@wizara_ya_kilimo
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai