Katika kuadhimisha siku ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani, wananchi wamejitokeza katika viwanja vya Snow View, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, kushiriki katika madhimisho siku ya Watoto wenye ulemavu wa Kichwa kikubwa na mgongo wazi lengo kuelimisha jamii na kuhamasisha upendo kwa watoto wenye ulemavu huu wa kuzaliwa.
Maadhimisho haya yameandaliwa kwa shirika la asbaht kushirikiana na serikali na Chama cha Wazazi Wenye Watoto Wenye Ulemavu wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, mgeni rasmi kutoka muwakirishi wa mkuu wa wilaya ya hai amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutoa huduma za upasuaji na matibabu kwa watoto wenye changamoto hizi kupitia taasisi kama MOI na hospitali za rufaa nchini zinatoa huduma .
Aidha, amewataka wazazi kutambua kuwa hali hizi si laana bali ni matatizo ya kiafya yanayoweza kutibiwa mapema iwapo jamii itakuwa na uelewa sahihi.
Kwa upande wao,Wazazi na walezi waliotoa ushuhuda wao walieleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwemo unyanyapaa, gharama za matibabu, na ukosefu wa vifaa saidizi.
Hata hivyo, wamemushukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk.samia Suluhu Hassan kwa kugharamia matibabu ya watoto zaidi ya 100 kupitia mpango maalum wa serikali, hatua iliyowapa matumaini mapya ya maisha bora kwa watoto wao.
Maadhimisho haya yamehitimishwa kwa sote tunawajibu wa kupunguza walemavu wenye kichw kikubw na mgongo wazi a kichwa kikubwa siyo laana Kauli hii imelenga kuvunja unyanyapaa na kuhimiza mshikamano wa kijamii katika kusaidia watoto hawa kufikia ndoto zao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai