Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh. Hassan Bomboko amekutana na kuzungumza na wafanyabiashara waliopo ndani ya stendi ya mabasi ya Boma’ngombe katika mkutano maalum ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai.
Katika Mkutano huo wafanyabiashara walipata nafasi yakueleza changamoto zao nakusikilizwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai kabla ya Mkuu wa Wilaya kujibu changamoto zao, baadhi ya wafanyabiashara wa ndani ya stendi ya Mabasi wameeleza sababu zilizowafanya kuongeza sehemu ya mbele ya biashara zao wakidai kuwa nikutokana na ongezeko la ukubwa wa biashara pamoja na eneo wanalofanyia biashara.
Baada yakusikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara Mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko amewaambia wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya awamu ya sita inawajali sana wafanyabiashara na lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wanafanya kazi katika mazingira salama ili kukuza biashara zao na vipato vyao visonge mbele, lakini pia DC Bomboko amewataka wafanyabiashara kuwa na mawazo mbadala ya kuziangalia fursa zingine za maeneo ya kufanya biashara wilayani hapo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai