Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Hai ambaye pia ni Afisa Kilimo wilaya David Lekei amewataka vijana kuchangamkia fursa kwenye Kilimo hasa cha umwagiliaji.
Lekei ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwaajili ya elimu ya Udhibiti ubora wa mbegu za maharage lishe, kupitia mradi wa Youth Entrepreneurship for the future of food and agriculture (YEFFA) unaosimamiwa na Tanzania Official Seed Certification Institute (TOSCI).
Amewataka vijana hao Kutumia vema fursa zinazotokana na kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kipato Kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
ANae Afisa lishe Mkoa wa Kilimanjaro Rehema Napegwa ameeleza umuhimu wa lishe hasa kwa akina mama na watoto, amesema mkoa wa Kilimanjaro una asilimia 20 sawa na watoto 48,000 wanahali ya udumavu jambo linalosababishwa na lishe duni.
Amewaasa jamii kuzingatia makundi yote sita ya vyakula ikiwemo jamii ya maharage lishe, ili kutenganisha kati ya nyama na maharage lazima tutumie vyakula mchanganyiko kwasababu maharage yana protein kama nyama lakn nyama ina mafuta mengi ganayosababisha uzito uliopitiliza
Afisa lishe wilaya ya Hai Silvania Kulaya amesema lishe ni muhimu hasa kwa wanawake wajawazito na wanaoenda kujifungua.
Kwa upande wake Marium Mwambati ambaye ndie Meneja mradi wa YEFFA amesema mradi huu utakuwa na tija kwenye Kilimo kwasababu katika jamii yetu kimekuwa na shida ya mbegu Bora, kwahiyo elimu hii itasaidia vijana kuwa wakulima waziri katika uzalishaji wa maharage lishe ili kuzalisha na kuongeza kipato na kufanya Kilimo chenye tija.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai