Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Juma Irando amewataka waalimu na wanafunzi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya shule mbali mbali iliyojengwa Wilayani humo.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo jana Des 24 2021 wakati akikabidhiwa vyumba 6 vya madarasa na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo, vilivyo kamilika katika Shule ya Sekondari Hai, baada ya kujengwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na zile za Uvico 19.
"Leo tumetembelea na kupokea vyumba vya mdarasa kwenye shule mbali mbali Wilayani kwetu na vimekuwa tayari kwa matumizi ya wanafunzi wetu hapo Januari mwakani
Kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza,kikubwa ni kutunza madarasa hayo,kwani Serikali inatumia gharama kubwa kujenga haya madarasa"
"Itakuwa Jambo la ajabu kuanza kuyakarabati haya madarasa kwa muda mfupi,kwa wanafunzi kuvunja vioo ,kuvunja madirisha,milango ,kukwaruza ukuta na kuvunja madawati hii hatutakubali"alisema Irando
Irando amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, wanaripoti shuleni kwa muda uliopangwa ili waweze kuanza masomo kwa wakati.
Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo, Dionis Myinga, ameishukuru Serikali ya awamu ya 6 kwa kutoa fedha sh. Milion 860 zilizofanikisha ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa katika shule mbali mbali za Sekondari Wilayani humo.
"Ni kweli vyumba 43 katika shule mbalimbali za Sekondari vimekamilika kwa asilimia mia moja,tunampongenza Rais Samia Suluhuu Hasani kwa kutuletea hizi fedha, amewasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa wasiingie kwenye michango ya kujenga vyumba hivyo"amesema Myinga
Myinga ameongeza kuwa wilaya hiyo hapo awali ilikuwa na upungufu wa vyumba 60 vya madarasa kwa shule za Sekondari na kusema kuwa kukamilika kwa madarasa hayo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa adha hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edmund Rutaraka,ameeleza kuwa wamejiridhisha na kiwango cha usimamizi wa fedha hizo katika kutekeleza miradi.
Wananchi wa wilaya ya Hai akiwemo Meshaki Jackson ameishukuru Serikali kwa kuwafanikisha ujenzi wa shule hizo tangu hatua ya boma hadi umaliziaji tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanachangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai