Mbunge wa Jimbo la Hai, Mheshimiwa Saashisha Mafue, ameimba Serikali kufanyia ukarabati barabara inayounganisha maeneo ya Rundugai, Kambi ya Chokaa mpaka Simanjiro, ambayo kwa sasa haipitiki kutokana na uharibifu unaosababishwa na mvua.
Mbunge Mafue amesisitiza kuwa hali hii imevuruga mawasiliano kati ya Wilaya za Hai na Simanjiro na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi katika maeneo haya muhimu.
Akijibu kuhusu changamoto hii, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Zainab Katimba, amesema Serikali inatambua mazingira hayo na inajitahidi kushughulikia matatizo yanayojitokeza kutokana na mvua na uharibifu wa barabara.
Aidha, Naibu Waziri Katimba ameitaka TARURA mkoa wa Kilimanjaro kwa ushirikiano na mameneja wa Manyara na wilaya husika kuhakikisha tathmini ya kina ya uharibifu wa barabara hiyo inafanyika haraka ili kuandaa maombi ya fedha kwa ajili ya hatua za dharura za kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo muhimu.
“Naagiza meneja wa TARURA mkoa wa Kilimanjaro akishirikiana na mameneja wa Manyara na wilaya hizi mbili kuhakikisha tathmini ya kina inafanywa na maombi ya fedha ya dharura yapelekwe ili kurejesha mawasiliano katika barabara hii muhimu inayounganisha wilaya hizi mbili,” amesema Naibu Waziri.
Serikali inasisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya barabara kuhakikisha mawasiliano na shughuli za maendeleo hayakatiki katika wilaya mbalimbali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai