wakazi wa Hai wametakiwa kujitokeza kufanya mazoezi kuimarisha afya zao kwa ujumla kwani afya ndio mtaji wa kwanza wa mafanikio.
Wito huo umetolewa hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Kuhusu uzinduzi wa program mpya ya mzoezi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 1 mwezi wa pili 2025.
Amesema kuwa lengo kubwa la mazoezi hayo ni kuimarisha afya ya mwili pamoja na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa presha na kisukari.
Ameongeza kuwa mazoezi hayo ya kukimbia na mazoezi ya viungo yana lengo la kuunga mkono jitihada za rais Samia suluhu Hasan za kufanya mazoezi kwa ajili ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na kuimarisha afya.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai