DC,HAI AWATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA MIRADI
Mkuu Wa Wilaya ya Hai Mhe.Lazaro Twange ametembelea miradi ya maendeleo inayo endelea kutekelezwa ,miradi hiyo ikiwa ni pamoja na Shule ya Msingi Msamadi na Sekondari ya Mbatakero Leo januari 22, 2025.
Akizungumza Katika ziara hiyo Mhe. Twange amewataka wakandarasi wenye jukumu lakutekeleza miradi kuhakikisha wanafanya kazi kwa biidi lengo kuu ni kumaliza miradi hiyo ndani ya mkataba na wakati sahihi.
Sambamba na hayo Mhe. Twange amewasisitiza wasimamizi wa miradi kusimamia miradi vyema kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inatelekezwa kwa ubora nzuri.
Pia Mhe. Lazaro ametaka Mwenyekiti wa Kijiji Mbatakero kuhamasisha upandaji wa miti pamoja na mau Katika maeneo ya mradi ili kujenga na kuboresha Hali ya kimazingira yanayo izunguka Shule hiyo.
"Hakikisha unahimiza upandaji wa miti Katika maeneo haya ambapo mradi unaendea sambamba na upandaji wa mauwa ni kuboresha mazingara yanayo izunguka mradi huu amesema Twange".
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai