Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imethibitisha kuwa inaendelea na jitihada madhubuti kuhakikisha zao la parachichi linapata soko la uhakika na la wakati kwa wakulima nchini, ikiwemo wakulima wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Hatua hiyo imekuja kufuatia swali lililoulizwa bungeni na Mbunge wa Jimbo la Hai, aliyehoji mpango wa Serikali katika kuhakikisha wakulima wa parachichi wanapata masoko yenye tija kwa maendeleo ya kilimo hicho kinachokua kwa kasi nchini.
Katika majibu ya Serikali yaliyotolewa bungeni leo, imeelezwa kuwa miongoni mwa mikakati iliyopo ni ujenzi wa vituo vya kisasa vya kuhifadhi mazao ya wakulima kabla ya kuyapeleka sokoni. Vituo hivyo vitajengwa katika maeneo yote yanayolima parachichi ili kusaidia wakulima kuepuka hasara zinazotokana na upotevu wa mazao au kukosa soko la haraka.
Aidha, Serikali imeeleza kuwa tayari imesaini mikataba na baadhi ya nchi kwa ajili ya kuuza parachichi kutoka Tanzania, na kwamba kampuni mbalimbali zimeingia makubaliano ya kununua parachichi moja kwa moja kutoka kwa wakulima katika maeneo tofauti nchini, ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Hai.
Mpango huu ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuinua kilimo cha mazao ya biashara na kuwainua wakulima kiuchumi kupitia ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai