Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Kituo cha Afya cha Kata ya Kia, wilaya Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Tukio hilo muhimu limefanywa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2025, Ismail Ali Usi ambaye alisifu juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wananchi katika kuboresha huduma za afya nchini.
Mradi huo wa ujenzi wa jengo la kisasa la OPD umegharimu zaidi ya shilingi milioni 200 hadi sasa, fedha zilizotokana na mchango wa serikali pamoja na nguvu za wananchi.
Jengo hilo linatarajiwa kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kata ya Kia na maeneo jirani kwa kutoa huduma bora, za haraka na kwa mazingira rafiki kwa wagonjwa.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi, Kiongozi wa mbio za mwenge Ismail Ali Ussi amewataka wananchi kuendelea kulinda miundombinu hiyo na kushiriki kikamilifu katika kuimarisha sekta ya afya.
"Ndugu zangu kabla ya kuwepo kwa kituo hiki,ni kweli kwamba wananchi walikuwa wakipata changamoto kubwa katika kupata huduma ya afya,lakini serikali sikivu iliona ipo haja ya kujenga kituo hiki cha Afya hivyo ni jukumu lenu sasa kulinda na kutunza miondombinu hii" Amesema Kiongozi wa mbio za mwenge Ismail Ussi"
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Kia wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea kituo hiki cha afya kwani walikuwa wakitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za afya lakini kwa sasa huduma hiyo inapatikana katika eneo lao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai