Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amempongeza raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa alizofanya ndani ya miaka minne ya utawala wa serikali ya awamu ya tano.
Akizungumza hii leo na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya maji Hai,amesema kuwa Dokta John Pombe Magufuli amefanya mengi ya makubwa ya kustaajabisha na ambayo hayakutegemewa kufanyika kwa wakati huu ikiwa ni pamoja na kurudisha reli inayotoka Tanga hadi Arusha ambapo reli hiyo ilikuwa imepotea kwa muda mrefu.
Sanjari na hayo pia Sabaya amewasisitiza Vijana kushirikiana na viongozi katika ngazi mbalimbali ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo.
Aidha ameongeza kuwa serikali haipo tayari kufumbia macho watu wanaojitokeza na kubeza kazi iliyofanwa na serikali ya awamu ya tano.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai