Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Yohana Sintoo amewataka watumishi wa Umma kwenye halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi huku wakimtanguliza Mungu katika majukumu yao.
Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha mwanzo wa wiki Sintoo amesema amefurahishwa na namna watumishi wa halmashauri hiyo walivyojituma kwa uaminifu kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 28 Octoba.
Sintoo amewapongeza watumishi wote walioshiriki zoezi hilo muhimu la kitaifa kwa kutekeleza majukumu mbalimbali kulingana na kada zao lakini zaidi kwa kujitoa bila kujali muda wa kazi na wengine kulazimika kufanya kazi kwa kukesha usiku mzima.
Sintoo ametambua utendaji wa watumishi akiwemo Aseri Mshangila dereva wa Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Floriana Dismas mtumishi wa kujitolea katika Idara ya Elimu Msingi kwa kuonesha utendaji uliotukuka na kuwazawadia kila mmoja fedha taslimu kiasi cha shilingi 20,000/= ikiwa ni motisha wa kujituma kwao na kuwa
Aidha Sintoo amewataka watumishi kufanya maandalizi kwa ajili ya kupokea na kuanza kufanya kazi na Baraza la Madiwani waliochaguliwa kwenye uchaguzi huo na kuwapa ushirikiano unaohitajika.
Awali Afisa Mipango wa Halmashauri Herick Marisham amewakumbusha watumishi kuhusu maandalizi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika idara zao, mpango mkakati wa miaka mitano na bajeti ikiwa ni hatua za mwanzo za utekelezaji wa kazi za Serikali kama zilivyoahidiwa kwenye kampeni za Rais, Mbunge na Madiwani kwa miaka mitano ijayo ya 2020 hadi 2025.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai