Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka watumishi wa Umma kwenye halmashauri yake kujikita katika kuwahudumia wananchi wanaopata huduma katika idara zao.
Sintoo ametoa wito huo kwenye kikao na watumishi wa makao makuu ya halmashauri hiyo ambacho ni mahususi kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa majukumu ya watumishi wote.
Amesema watumishi wanatakiwa watambue kuwa uwepo wao kwenye ajira ni kwa ajili ya kutatua kero na matatizo yanayowakuta wananchi.
"Kazi kubwa tuliyonayo sisi watumishi wa umma ni kutatua kero za wananchi, mambo mengine yote yanafanyika ili kusaidia katika kufanikisha lengo kuu LA kutatua kero za wananchi" Amesema.
Amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kuandaa mpangokazi unaoendana na mahitaji ya wananchi ili kuwepo na utaratibu unaoeleweka wa kutatua kero za jamii kila wiki.
Mkurugenzi Mtendaji ameweka utaratibu wa kukutana na watumishi wote wa makao makuu ya halmashauri kila siku ya Jumatatu saa moja na nusu hadi saa mbili asubuhi ambapo hupokea na kujadili mpangokazi wa kila idara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 27 Hai
Simu: 0272758441
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai