• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

Madiwani Wakumbushwa Kusimamia Kimalifu Usimamizi Wa Mazingira

Imetumwa: March 10th, 2023

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utunzaji wa mazingira ikiwemo kuzuia ukataji holela wa miti unaosababisha  mabadiliko makubwa ya tabia nchi.


Rutaraka ambaye ni diwani wa kata ya Muungano wilayani humo amesema kuwa licha ya kwamba mchakato wa vibali vya ukataji miti vinapitia kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilayani lakini pia madiwani wanayo nafasi ya kusimama imara kuhakikisha ukataji wa miti kiholela unadhibitiwa.


Ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani  kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo kufuatia hoja iliyoibuliwa na diwani wa kata ya Mnadani Nasibu Mndeme ya kuweka msisitizo wa namna ya kusimamia utunzaji wa mazingira katika wilaya ya Hai.


"Hoja hii pamoja na kuletwa kwenye baraza letu, lakini tayari Mhe. Mkuu wa wilaya ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya tayari alishaanza kulishughulikia, kwahiyo sisi kwenye baraza tulileta ili kuweka msisitizo na madiwani wote waweze kuwa na lugha moja ya kuhakikisha wanasimamia mazingira"


Kwa upande wake katibu Tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka viongozi wa ngazi za chini wakiwemo watendaji na madiwani kuhakikisha wanachukua hatua za kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti usiofuata taratibu.


Naye mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dionis Myinga ameeleza kuwa jukumu la kutunza mazingira ni la kila mtu na kuwataka wananchi wote wa wilaya hiyo kushirikiana katika kutunza mazingira.


Katika hatua nyingine baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Hai limeunda kamati ndogo yenye wajumbe wanne ambayo imepewa mwezi mmoja kuchunguza vitendo vya uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji wilayani humo baada ya kusemekana kuwa kuna watu wamekuwa wakivamia na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kwenye vyanzo vya maji.


Wajumbe walioteuliwa kwenye kamati hiyo ni diwani wa kata ya Mnadani Nasibu Mndeme, diwani wa kata ya Masama Magharibi  Machoya Natai, pamoja na madiwani wa viti maalum Ausen Nkya na Upendo Sawe.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI YA FUNDI MKUU UJENZI March 17, 2023
  • KUITWA KAZINI January 23, 2023
  • TANGAZO LA KAZI, MKUSANYA MAPATO NA MTEKNOLOJIA MSAIDIZI DAWA January 24, 2023
  • TANGAZO LA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA January 25, 2023
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Madiwani Wakumbushwa Kusimamia Kimalifu Usimamizi Wa Mazingira

    March 10, 2023
  • TASAF Wilaya Ya Hai Yatoa Vifaa Vya Milioni 162

    March 06, 2023
  • Chama Cha Mapinduzi Chaahidi Kuendelea Kushirikiana Na Jeshi La Polisi Hai

    March 01, 2023
  • Kata Ya Masama Kusini Yaanza Ujenzi Wa Shule Ya Sekondari

    March 01, 2023
  • Ona Yote

Video

UGAWAJI WA PIKIPIKI WILAYA YA HAI
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • BARUA PEPE YA MALALAMIKO
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 27 Hai

    Simu: 0272758441

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai