Mbunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Saashisha Mafuwe amewataka madereva bajaji na boda boda wilayani Hai kushiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ifikapo Agosti 23, 2022.
Saashisha ametoa rai hiyo Julai 14 2022 wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa katiba ya umoja wa waendesha bajaji wilayani humo, katika ukumbi wa Bamboo uliopo Bomang'ombe.
"Niwaombe sana tarehe 23/08/2022 waendesha bajaji na pikipiki wote wilaya ya Hai chonde chonde tujitokeze kuhesabiwa, siku hiyo tutulie kwenye maeneo yetu tuhesabiwe"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 27 Hai
Simu: 0272758441
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai