Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Kiseo Nzowa ameupongeza uongozi wa wilaya ya Hai Kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na kuzuia hoja za ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Nzowa ametoa pongezi hizo Leo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwa kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri kilicho lenga kujadili taarifa za utekelezaji za robo ya nne.
Amesema mafanikio yanayopatika Hai yanatokana na ushirikiano uliopo Kati ya viongozi wote na kutaka ushirikiano Huo uendelee.
"Nawasihii Sana katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 muendelee kukusanya vema mapato na kuwa mfano Kwa halmashauri zingine".
"Pia baada ya kukusanya mjitahidi Sana kusimamia matumizi ya fedha hizo na kuzuia mianya yote ya upotevu wa fedha" amesema Nzowa.
Kwa upande wake Mkuu Wa Wilaya ya Hai amempongeza Katibu Tawala Kwa kuaminiwa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Ameahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majuku ya serikali ili kusudi la kuwafikishia huduma wananchi lifikiwe.
Halmashauri ya Wilaya ya Hai imefanikiwa kuvuka lengo katika ukusanyaji wa mapato Kwa kukusanya zaidi ya aslimia 100 mwaka 2023/2024 na kuzuia hoja ambapo ina hoja tano huku nyingi zikiwa ni za kisera na mfumo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai