Mashabiki wa klabu ya simba wilaya ya Hai wameishauri jamii kusaidia watu wenye wa mahitaji maluum kama wazee, wagonjwa na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mwenyekiti wa simba tawi la Hai Bw Fadhili Salimu ametoa rai hiyo wakati tawi hilo lilipo watembele wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Hai na kutoa misaada mbalimbali kwa akina mama na watoto.
‘’tumekuja kuwaona na kuwasalimia watoto wanaotibiwa katika hospitali hii ,kuchangia damu na kufanya usafi wa hospitali’’.
Aidha mmoja wa mashabiki wa klabu hiyo Bw Jumaah Mwilongo amesema wamefurahia zoezi hilo linalogusa maisha ya watanzania na kwamba ni sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya timu ya simba mwaka huu inayosema simba nguvu moja.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 27 Hai
Simu: 0272758441
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai