Kufuatia kusambaa kwa taarifa potofu kwenye mitandao ya jamii kuhusu shule ya msingi Mbosho iliyoko wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ikionesha jengo chakavu la shule hiyo na kwamba uchakavu huo umesababisha wazazi kuhamisha wanafunzi wao kwenda kwenye shule za Vijiji jirani,afisa habari wilayani Hai Riziki Lesuya ametoa ufuafanuzi kuhusiana na suala hilo .
Akizungumza na redio Boma Hai fm mapema leo ,amefafanua kuwa,shule ya msingi Mbosho ina jumla ya wanafunzi 138 na walimu 6 ambao wanatosheleza kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo, hivyo shule hii haina upungufu wa walimu na hakuna mwanafunzi yoyote aliehamia shule za Vijiji jirani kutokana na uchakavu wa shule ya hiyo.
Ameongeza kuwa Jengo lililopigwa picha linalo sambaa kwenye mitandao ya kijamii likionekana ni chakavu, si miongoni mwa vyuma vya madarasa bali ni jengo linalotumika kama stoo kwa ajili ya Samani chakavu.
Naye afisa elimu msingi Hidaya Kilima ameongeza kuwa Tangu kuingia madarakani Mwaka 2021 hadi 2025, serikali ya awamu ya Sita imetoa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya shule kongwe, ujenzi wa shule mpya za mkondo mmoja 4 na ujenzi wa zaidi ya vyumba vya madarasa 80 na matundu ya vyoo zaidi ya 341.
Ameongeza kuwa Shule za Msingi Mtakuja, Narumu Tela, Ishara Ufundi na Kyuu nazo zipo kwenye mpango wa mwaka 2025/2026 zinasubiri fedha kwa utekelezaji huku shule ya Msingi Mbosho, Mbwera, Kimbushi, Kyuu na Kware zinatarajiwa kuwekwa kwenye mpango wa bajeti wa mwaka 2026/2027.
Hata hivyo afisa habari wilayani Hai Riziki Lesuya amewasihi wananchi kupuuzia taaarifa zisizo sahihi zinazosambaa katika mitando ya kijamii badala yake pale wanapohitaji kupata taarifa yoyote inayohusu Halmashauri wafuate utaratibu wa kupata taarifa hizo kwenye vyanzo rasm
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai