• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

TASAF Yaandaa Wawezeshaji Wilaya ya Hai Kufanya Uhakiki wa Wanufaika

Imetumwa: July 14th, 2020

Wito umetolewa kwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakiwemo Wakuu wa Idara na wawezeshaji kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kutimiza malengo yaliyowekwa na Serikali katika kuhudumia wananchi wake.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa wakuu wa idara za halmashauri na wawezeshaji wa TASAF ngazi ya wilaya; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka watumishi wa Umma wanaoshiriki mafunzo hayo kuwa wasikivu ili ujuzi watakaoupata ukawasaidie kufanikisha malengo ya Serikali.

“Niwaombe ndugu zangu mnaopata mafunzo haya; kujifunza kwa umakini mkubwa na kwenda kutumia ujuzi mtakaoupata hapa kwa weledi na uaminifu mkubwa mkiweka mbele maslahi ya Taifa na huduma kwa wananchi wetu” Ameongeza Sintoo.

Akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Ladislaus Mwamanga; Makwinja Dismas amesema kuwa mafunzo watakayoyapata yamelenga kuwaongezea ujuzi wataalamu katika kutambua na kutoa taarifa sahihi za wanufaika wa miradi ya TASAF katika wilaya.

Amesema zoezi la kutambua walengwa linafanyika kwa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa kuzindua awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini huku akibainisha kuwa kumekuwa na taarifa za malalamiko kuwa wapo wanufaika ambao hawastahili kunufaika na mpango huo huku wakiwepo wenye uhitaji ambao hawajapata nafasi kwenye mpango huo.

Amesema kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF inategemea kuwafikia wanufaika Zaidi ya milioni 7 kwenye kaya milioni moja laki nne na nusu ikiwa ni nyongeza ya kaya laki tatu na nusu huku akibainisha kuwa awamu hii inaweka mkazo kwa kaya kufanya kazi ili kuongeza kipato.

Aidha Makwinja amekumbusha kuwa ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kama inavyoelekezwa na Wizara ya Afya kuhusu kunawa mikono kwa maji na sabuni, kuepuka misongamano pamoja na kukaa umbali wa mita mbili kati ya mtu mmoja na mwingine.

Kikao kazi hiki kinalengo la kuwaandaa wawezeshaji wa TASAF wa halmashauri ya wilaya ya Hai ikiwa ni maandalizi ya zoezi la uhakiki wa kaya zinazonufaika na Mradi wa Kunusuru Kaya Masikini.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UCHAGUZI MKUU 2020 October 10, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UCHAGUZI MKUU 2020 October 10, 2020
  • TANGAZO LA USIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI MWAKA 2020 October 20, 2020
  • Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo 2020 May 30, 2020
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Wanawake, Vijana jiungeni kwenye vikundi mnufaike na mikopo ya Serikali: Diwani Masama Kusini

    January 21, 2021
  • Diwani Bomang'ombe Aahidi Kusaidia Wenye Uhitaji, Ajira kwa Vijana

    January 12, 2021
  • 'Hai Rural Teachers SACOSS' Wapata Uongozi Mpya

    January 10, 2021
  • Mbunge wa Hai Akabidhi Vifaa Tiba Zahanati ya Kware

    January 09, 2021
  • Ona Yote

Video

Wilaya ya Hai Nafasi ya 4 Kitaifa Darasa la Saba 2020
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri nje ya nchi

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 27 Hai

    Simu: 0272758441

    Simu ya Mkononi: 0752195133

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai