Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe Saashisha Mafuwe amewataka wataalamu wa maji wilaya ya Hai kusimamia na kutatua changamoto zinazosababisha uhaba wa maji katika maeneo kadhaa ya wilaya ya Hai.
Ametoa wito kwa viongozi wa serikali kuwatafuta wakandarasi wote ambao hawajakamilisha miradi ya maji,kutokana na uzembe wakutoweka mbele miradi ya maji nakuwachukulia hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kusitisha mikataba Yao kama hawana uwezo wakukamilisha miradi kwa wakati na Kwa ubora unaotakiwa
Mafuwe amewataka wataalamu wa maji na wakandarasi kufika katika maeneo ya kazi zao( sights) ili kukamilisha miradi ya maji kwa wakati, ameongeza kuwa hatosita kusitisha mikataba endapo uzembe utaendelea.
Nae Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe Hassan Bomboko ametoa wiki mbili kukamilisha Mradi wa Maji kikafu Soka awamu ya pili unaotoa maji kikafu hadi kwenye tenki jipya la Matowo na kupeleka kwenye tenki la Kwasadala kuelekea Bomang'ombe katika wilaya ya Hai.
Vilevile ameagiza bodi ya maji kuzuia kuuza maji nje ya wilaya ya Hai kwa kipindi hiki mpaka suluhisho la maji lipatikane katika maeneo yote yasiyo na maji yakutosha.
Katika wilaya ya Hai Kuna uhitaji wa lita milioni 30 na sasa inazalisha Lita milioni 27 jambo ambalo linaashiria hakuna uhaba mkubwa sana wa maji Kwa Sasa tofauti na kipindi cha nyuma ambacho hapakuwa na maji kabisa.
Kwa Sasa kwenye kata tatu za mamlaka ya mji Mdogo wa Bomang'ombe Kuna uhitaji wa lita milioni 1.4 kwa siku, ahadi ya serikali kwakushirikana na mkandarasi kufikia Desemba 31,2025 Uhaba wa maji Kwa mji mdogo wa Bomang'ombe utakuwa umekwisha.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai