• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Accounts and Finance
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

Mkurugenzi Hai Awataka Watendaji Kata Vijiji Kudhibiti Wageni Kupambana na Corona

Imetumwa: April 8th, 2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai amewaagiza Watendaji Kata na Vijiji katika halmashauri hiyo kuweka utaratibu wa kufuatilia na kutoa taarifa za watu wanaoingia kwenye maeneo yao ikiwa ni jitihada za kujikinga na ugonjwa wa Homa Kali ya mapafu wa Corona.

Sintoo ametoa maelekezo hayo pamoja na barua kwa watendaji wakati akipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu wa Corona wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni moja wenye vifaa kama ndoo 17 za kunawia mikono pamoja na sabuni kutoka Taasisi ya Kijana Kwanza ya mkoani Kilimanjaro.

“Watendaji wa ngazi zote, hakikisheni hakuna mtu anayeingia kinyemela kwenye maeneo yenu; wekeni mtandao wa taarifa kwa kuwashirikisha mabalozi wa nyumba pamoja na wananchi kwa ujumla kuwapa taarifa ya wageni” amesema Sintoo.

Sintoo ameongeza kuwa Wilaya ya Hai ni moja kati ya wilaya zenye mwingiliano mkubwa wa watu hapa nchini ikichangiwa na uwepo wa kiwanja cha ndege, barabara kuu ya lami inayounganisha mikoa pamoja na kuwa karibu na mipaka ya nchi huku akiwashukuru wananchi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa taarifa juu ya watu wanaohisiwa kuingia nchini kinyemela wakikwepa maelekezo ya Serikali na kusema kuwa kufanya hivyo kunazidi kuonesha umakini walionao wananchi wa wilaya ya Hai.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi Kijana Kwanza Mujibu Idrisa amesema kuwa taasisi yao imeona ni vyema kutoa mchango wake wenye kuisaidia jamii kwa kupata ndoo za maji kwa ajili ya kila ofisi ya kata huku akiitaka jamii ione kuwa mapambano dhidi ya janga la CORONA yanapaswa kufanywa na kila mtu ili kuhakikisha maambukizi hayaendelei kusambaa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Machame Magharibi Martini Munisi akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Hai amesema kuwa msaada huo unazidi kuonesha juhudi za makusudi kutoka katika taasisi mbalimbali za kupambana na Corona huku akiipongeza kamati Wilaya ya kupambana na ugonjwa huo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai  Ole Sabaya akishirikiana na katibu wake Dkt. Irene Haule kwa kufanya kazi usiku na mchana na namna wanavyoshughulikia taarifa zinazotolewa na wananchi kuhusiana na mapambano ya ugonjwa huo.

Zoezi la kugawa vifaa hivyo ni mwendelezo wa hatua zinazochukuliwa katika Wilaya ya Hai kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujikinga, kuelekeza wafanya biashara na watoa huduma kuweka vifaa vya kunawia mikono kwenye maeneo yao, kuweka maji na sabuni kwenye mageti ya halmashauri na ofisi zilizo chini yake pamoja na vitakasa mikono kwenye milango ya kuingia ofisi za halmashauri

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA UDEREVA, MWANDISHI MWENDESHA OFISI, MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU NA MHUDUMU WA JIKONI June 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA YA UDEREVA March 28, 2025
  • TANGAZO LA MKOPO KWA WATUMISHI December 20, 2024
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA JIMBO LA HAI 2024 December 03, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Serikali Kuboresha Soko La Parachichi

    June 11, 2025
  • Ng'ombe Elfu 88 Kupata Chanjo Ya Mapafu Wilayani Hai

    June 12, 2025
  • Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Yametakiwa Kushirikiana

    June 10, 2025
  • Mbunge Wa Jimbo La Hai Aomba Matengenezo Ya Barabara

    June 10, 2025
  • Ona Yote

Video

UGAWAJI WA PIKIPIKI WILAYA YA HAI
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • BARUA PEPE YA MALALAMIKO
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai

    Simu: 0754553560

    Simu ya Mkononi: 0754553560

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai