Madiwani wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vema uendeshaji wa shughuli za serikali za mtaa katika halmashauri ya wilaya ya Hai ili kujenga halmashauri yenye hati safi kwa kipindi chote cha miaka mitano.
Hayo yameainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Edmund Rutaraka wakati akifunga rasmi mafunzo ya Madiwani yaliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Halmashauri ya Hai.
Rutaraka amesema mafunzo hayo yatawasaidia Madiwani kufahamu majukumu yao kikamilifu na namna ya kusimamia utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali katika kata zao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Masama Kusini Cedric Pangani, amesema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu nafasi ya madiwani katika kuimarisha demokrasia ya ndani na mahusiano bora na wananchi.
Amesema mafunzo hayo pia yanalenga kuwajulisha wananchi kuhusu uwajibikaji wa mabalozi wa mtaa, kwa kuhakikisha wananchi wanatoa taarifa za wageni wanaoingia kwenye mtaa ili kujulikana katika kaya husika na kuimarisha usalama wa wananchi wa mtaa au kata husika.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai